Changamoto za wafanya biashara wa madini kutatuliwa

Serikali imeahidi kutoa kipaumbele kwenye changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa madini nchini, ili kuwezesha sekta hiyo kutoa mchango mkubwa kwa Taifa.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema hayo alipokutana na wafanyabiashara wa madini wa soko la madini Kahama, kwa lengo la kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi.

“Mtakumbuka niliwahi kufika hapa Kahama kwa changamoto ya utoroshaji, lakini niliwaahidi kuwa nitatenga siku maalumu ili nije niwasikilize changamoto zenu na kwa pamoja tushauriane namna bora ya kuzitatua kwa masilahi mapana ya nchi yetu na sekta ya madini kwa ujumla.”

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo mahususi ya kusimamia sekta ya madini kikamilifu na kuhakikisha changamoto zinazowakabili wachimbaji na wafanyabiashara ya madini zinatatuliwa.


Waziri Mavunde amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha inafuatilia kwa ukaribu na kusimamia sekta ya madini ili kubaini iwapo changamoto zilizopo ni za kiusimamizi au mfumo.

Amesema lengo ni kuona kama changamoto zinasababishwa na sheria ili Serikali ifuate taratibu za kupeleka bungeni mapendekezo ya kubadili sheria na kuinua zaidi biashara ya madini nchini.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *