Kutoa Meno ni hatua ya mwisho-Mwakasege

Daktari wa afya ya kinywa na meno Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Rhoda Mwakasege amesema utafiti unaonyesha watoto wenye umri wa miaka sita hadi tisa ni waathiriwa wakubwa wa magonjwa ya meno.

Doktari Mwakasege Amesema hayo baada ya Wananchi Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi kuonyesha uhitaji wa elimu ya kutosha juu ya utunzaji wa kinywa na meno.

Amewataka wananchi kutokukimbilia kutoa meno pindi wanapopata changamoto ya meno bila kufanya matibabu na kwamba kutoa meno ni hatua ya mwisho baada ya matibabu kushindikana.

Aidha wananchi wameshauriwa kufika katika vituo vyaafya pindi wanapo gundua changamoto

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *