Putin kukutana na Xi Jinping

Rais wa Urusi Vladimir Putin mwezi Mei anatazamiwa kuelekea chini China kukutana kwa mazungumzo na Rais Xi Jinping, katika ziara inaweza kuwa ya kwanza nje ya nchi katika muhula wake mpya wa urais.

Serikali za magharibi zimekosoa kuchaguliwa kwa Putin na  mchakato wa uchaguzi haukuwa huru, wala wa kidemokrasia. Lakini China, India na Korea Kaskazini zilimpongeza kiongozi huyo ambaye pia ni mshirika wao, kwa kuendeleza utawala wake kwa miaka sita zaidi.

Sherehe rasmi za kuapishwa Putin zinatarajiwa kufanyika Mei 7 mwaka huu.

Katika miaka ya hivi karibuni, China imeimarisha uhusiano wake wa kibiashara na kijeshi na Urusi, huku Marekani na washirika wake wakiziwekea vikwazo nchi hizo mbili, haswa Moscow, kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine.

Ikumbukwa kuwa Putin ataendelea kuliongoza taifa hilo baada ya kushinda asilimia 87.54 ya kura baada ya asilimia 99 ya kura kuhesabiwa ambapo Watu milioni 76 walimpigia kura Putin.

Hatahivyo Ujerumani, Uingereza, Italia, Jamhuri ya Czech pamoja na shirika la usalama na ushirikiano barani  Ulaya OSCE, zimesema uchaguzi uliofanyika haukuwa huru wala wa  haki na uliwanyima raia wa Urusi, nafasi huru ya kumchagua wanaemtaka.

Nae rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameonyesha kutofurahishwa na ushindi wa Putin na kuuelezea uchaguzi kutokuwa halali, na akaenda mbali zaidi kusema Putin amelewa madaraka na atafanya kila mbinu ya kuendelea kuongoza milele.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *