Uhusiano wa Tanzania na Ujerumani una tija kimaendeleo

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza Hassan Masala amesema uhusiano baina ya Ujerumani na Tanzania ulioanza tangu mwaka 1960 umekuwa na tija kutokana na kuwepo miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

Masala amesema hayo leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, akimpokea balozi wa Ujerumani Thomas Terstegen

Amebainisha kuwa miradi iliyoletwa na Ujerumani hususani sekta ya Afya, Umeme, Maji, MaliAsili, na Elimu imekuwa chachu ya maendeleo hapa nchini.

“Mhe. Balozi nikushukuru kwa kuutambua Mkoa wa Mwanza upo kimkakati na kuleta miradi ya afya,maji na mazingira hii ni hatua nzuri ambayo itazidi kuuimarisha kiuchumi mkoa huu,” amesema Masala.

Nae Balozi wa Ujerumani Mhe.Thomas Terstegen amesema uhusiano wa Tanzania na Ujerumani utazidi kuwa endelevu huku ukiwanufaisha wananchi wa pande zote mbili.

“Kutokana na jiographia ya Mwanza tutaleta Mradi wa kuimarisha mifumo ya maji taka na safi kwa wanaoishi sehemu za milimani, pia tutajenga kingo za mto mirongo na kuleta vifaa vya kupambana na uchafuzi wa mazingira.” amesema Balozi Terstegen

Katika ziara yake ya siku moja Jijini Mwanza atatembelea Chuo cha wanyamapori cha Pasinsi, ikiwa ni miongoni mwa miradi wanayoifadhili.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *