Wanafunzi wachapwa viboko 75, wakimbizwa hospitali.

Wanafunzi 12 katika shule ya  Sekondari Ipandikilo  Iliyopo Kata ya Ngoma B  Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza   wamedaiwa   kuchapwa viboko 75 na baadhi ya walimu wa shule hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na mapenzi shuleni.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wanafunzi wakiwa  katika kituo cha afya  Ngoma B  wamesema kuwa baada ya kutuhumiwa kujihusiha na mapenzi , walimu walianza kuwachapa viboko kwa zamu na kupelekea  kupata maumivu makali   sehemu mbalimbali za miili yao .

Mkuu wa shule ya sekondari Ipandikilo  Mwl, John Paul amesema wameshirikiana na afisa mtendaji wa kata hiyo kuwapeleka kwenye kituo cha afya wanafunzi hao kwa ajili ya kupatiwa matibabu wakati  taratibu nyingine zikiendelea.

Nae Mganga mfawidhi wa  Kituo cha afya Ngoma B  Abtwalib Nkwaje  amethibitisha kuwapokea  wanafunzi  katika kituo hicho cha afya huku wakiwa na michubuko sehemu mbalimbali za milii yao. 

Afisa mtendaji wa kata ya Ngoma B    Emily John  amesema   Ofisi yake imepokea  malalamiko kutoka kwa wazazi wakiwa na watoto wao  kwa kupewa adhabu zilizokithiri na kumtaka mkuu wa shule hiyo  kutoa maelezo juu ya  tukio hilo.

Diwani wa kata ya Ngoma B  Donald Masindi  amesema kitendo hicho hakiwezi kuvumiliwa na kushauri walimu wanaodaiwa kufanya kitendo hicho kuchukuliwa hatua za kinidamu.

Kufuatia tukio hilo  Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Sengerema Jackson Mazinzi  na katibu wa Jumuiya hiyo Jamal  Athuman  wamewatembelea wanafunzi katika kituo hicho cha afya na kuagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa mkuu wa shule hiyo ili kukomesha vitendo hivyo.

Aidha Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wanaodaiwa  kuchapwa viboko  wameiomba serikali kuwaondoa shuleni hapo  walimu  walio tekeleza kitendo hicho.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *