Wawili Kortini kwa kughushi nyaraka

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bukandwe mkoani Geita, Ambakisye Mfwango na mwenzake Beatrice Musiba wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Geita wakishtakiwa kwa makosa ya ubadhilifu wa mali za umma na kughushi hati za malipo yenye thamani ya Sh1.5 milioni kinyume na sheria.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kusomewa mashtaka na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Chali Kadeghe mbele ya Hakimu Benson Fungo.

Katika shauri hilo la rushwa na uhujumu uchumi, washtakiwa hao kwa pamoja wanashtakiwa kwa kughushi nyaraka za vikao vya Kamati ya Shule ya Msingi Kanegere.

Washtakiwa hao wamekana makosa hayo na mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye ni mtumishi wa Serikali atakayesaini hati ya Sh2.5 milioni.

Aidha Kesi yao imeahirishwa hadi Machi 28, 2024 itakapoitwa kwa ajili ya upande wa mashtaka kusoma hoja za awali.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *