Wazazi wa kiume wametakiwa kuwajali Watoto wenye ulemavu wa ngozi kwa kuhakikisha wanapata elimu bora.
Rai hiyo imetolewa na Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mitindo iliyopo Jijini Mwanza ambayo pia inahudumia watoto wenye ulemavu wa ngozi Mwl. Januari Gunze.
Mwl. Gunze amesema wamekuwa wakipokea watoto kutoka kwa wakinamama ambao wameachiwa majukumu ya kuwalea watoto hao kutokana na dhana potofu.
”Hata miongoni mwa hawa watoto tunao wapokea hapa, maranyingi unakuta ni mzazi mmoja sanasana unakuta ni mzazi wa kike, upande wa mzazi wa kiume anapojifungua mama mtoto mwenye ualbino anamkimbia, anamtelekeza kwahiyo tunaendelea kupokea hao watoto wenye changamoto hizo unakuta ni familia ya single mama kwahiyo hata mpaka sasa wapo”amesema mwl. Gunze.
Amesema watoto hao wanauelewa mzuri darasani na wanaweza kufanya vizuri hivyo ni wajibu wa wazazi kufuatilia maendeleo yake na kumpa malezi yanayo stahili.