Waandishi wa Habari wa Afya Radio wametakiwa kuzingatia usawa wa kijinsia katika kuandaa maudhui yao.
Mkufunzi wa chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino Mwanza (SAUT) Nuru Chuo amesema hayo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi hao kuhusiana na maswala ya kijinsia katika uandaaji wa maudhui.
Kwa upande wake Mhariri Mkuu wa Afya Radio Feliciana Manyanda amesema ni muhimu kuzingatia jinsia wakati wa kuandaa Habari ili kuweka usawa katika jamii
”sisi tupo kama sauti ya watu ambayo haina sauti nikimaanisha kwamba ndo ile jamii ambayo tunaihudumia sisi kama Afya Radio” amesema Feliciana
Waandishi wa habari wa @afyafm pia wametakiwa kuripoti habari za ukatili kwa kuzingatia maadili.
Amewataka waandishi kupunguza ukali wa maneno wanaporipoti matukio hayo na kutotumia lugha za utani.