Mkurugenzi wa mamlaka ya kudhibiti wa huduma za nishati kanda ya ziwa EWURA George Mhina amesema watanzania wanaoishi maeneo ya vijijini wanamatumizi makubwa ya nishati chafu ikiwemo kuni na mkaa na huwaathiri zaidi wanawake
Amesema hayo wakati akizungumza na afyaradio kuhusu athari za matumizi ya nishati chafu nakwamba matumizi ya nishati chafu pia huchangia vifo kwa wanawake.
Pia amesema katika harakati za kutafuta kuni kwaajili ya matumizi ya kupikia kunaweza kusababisha wanawake kukutana na vitendo vya ukatili kwani upatikanaji wa nishati hiyo sio salama.
Amesema serikali imekuja na mkakati wa miaka kumi kuhamasisha nishatai safi ya kupikia ili kuwanusuru wanawake na kuepusha athari za kimazingira zinazoweza kusababishwa na matumiazi ya nishati chafu.