NISHATI CHAFU SI RAFIKI KWA AFYA-KITOGO

Inaelezwa kuwa nishati chafu si Rafiki kwa afya ya binadamu na mazingira kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Afisa mazingira katika shirika la EMEDO lililopo jijini Mwanza, Kitogo Laurence akizungumza na Afya Redio kuhusiana na Athari za matumizi ya nishati chafu ikizingatiwa wanawake ndio wanaotumia kwa wingi kwenye shughuli mbali mbali.

Nao baadhi ya wananchi wamesema si kila mtanzania anaweza kumiliki gesi au umeme, hivyo athari zitaendelea kuwepo kutokana na matumizi ya nishati chafu na gharama kubwa za kuipata nishati safi.

Sera ya Taifa ya Afya ya Mwaka 2007, inaelekeza kuwapo utaratibu mzuri na endelevu kuhifadhi, kutunza na kulinda mazingira kwa faida ya afya ya wanachi na vizazi vijavyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *