Baadhi ya wanawake waliojitosa kuwania uongozi wa kisiasa, wamesema wamekumbana na udhalilishaji mtandaoni, wakiitaja mitandao ya kijamii kuwa sumu kwa wanawake kisiasa.
Wakina mama hao wamesisitiza kuwa aina hiyo ya udhalilishaji ni miongoni mwa mambo yanayorudisha nyuma mikakati ya kitaifa inayolenga kufikia usawa wa kijinsia katika siasa.
Takwimu rasmi za kiserikali zinaonesha kundi hilo bado halina uwakilishi mkubwa kwenye vyombo vya uamuzi.