Wazazi wametakiwa kuwashika mkono Watoto wa kike katika safari ya masomo ili kutimiza malengo yao.
Wito huo umetolewa na Hakimu Witness Ndoss wakati akizungumza na afya radio juu ya changamoto zinazo wakabili Watoto wakiki pindi wanapochagua kusomea masomo yanayo yafanya kufikia kuwa hakimu.
Amesema vijana wakike wanashindwa kufikia ndoto zao kutokana na kukosa kuungwa mkono katika masomo yao pamoja na kujii ngiza kwenye makundi yasiyo faa pindi wanapofika vyuoni
Amesema ili kijana wa kike aweza kufikia ndoto zake ni vema kujua nini anacho kifanya awapo chuoni na kuacha kufuata mikumbo ya watu yanayoweza kusababisha kushindwa kufikia malengo yake.
Hakimu ndosi pia amesema mwanamke hakimu anauwezo wa kufanya maamuzi sawa na anavyoweza kufanya mwanaume licha ya baadhi ya watu kujijengea thana potofu kuwa ni vigumu kwa mwanamke kuwa hakimu.