NHIF YAFANYA MABORESHO, VIFURUSHI SASA NI SERENGETI NA NGORONGORO

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Mwanza Jarlath Mushashu amewataka wananchi kukata bima mapema kwani ni muhimu kuwa na Bima ya afya.

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Mwanza Jarlath Mushashu akielezea maboresho ya NHIF katika kituo cha radio @afyaradio Kilichopo Jijini Mwanza.

Akielezea maboresho ya mifumo mipya katika bima hiyo Mushashu amesema kwa sasa vifurushi ni Viwili tofauti na hapo awali.

Afisa udhibiti Ubora NHIF Mkoa wa Mwanza Obedi Kabinza akielezea lengo la maboresho ya bima ya NHIF katika kituo cha radio @afyaradio Kilichopo Jijini Mwanza.

Kwa upande wake Afisa udhibiti Ubora NHIF Mkoa wa Mwanza Obedi Kabinza amesema maboresho hayo yamefanyika ili kuleta ufanisi katika utoaji huduma za bima Nchini Kupitia vifurushi hivyo vipya.

Amesema vifurushi hivyo vimezingatia maboresho ya huduma za sekta za Afya nchini na kuweka huduma ambazo hazikuwepo katika vifurushi vya awali

Amevitaja vifurushi hivyo vipya ambavyo ni viwili ni Ngorongoro Afya Na Serengeti Afya ambapo zamani kulikuwa na vifurushi vitatu ambavyo ni Najali Afya Wekeza Afya na Timiza Afya ikiwa ni kutangaza utalii Nchini na kuonesha utofauti wa Mbuga hizo Mbili

Amesema Ngorongoro Afya ina Huduma 445 na Serengeti Afya 1815 ambapo mtanzania anaweza kuchagua kujiunga kulingana na Uwezo wa kifedha.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *