NI MUHIMU VIJANA KUELEWA AFYA YA UZAZI-MOKIWA

Imeelezwa kuwa ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana hasa wa kiume kunawapelekea kushindwa kufikia malengo yao.

Hayo yameelezwa na Afisa ustawi wa jamii halmashauri ya Jiji la Mwanza Edith Mokiwa na kwamba wamekuwa wakipokea kesi za watu kushindwa kuhudumia familia zao ikiwa ni matokeo ya kukosa elimu hiyo.

Amesema wao kama ustawi wa jamii wanafanya jitihada za kutoa elimu kwa vijana juu ya umuhimu wa kuwa na elimu ya afya ya uzazi.

Kwa upande wake Kaimu Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Buzuruga daktarai Poul Godfrey amesema elimu ya afya ya uzazi ni muhimu kwani ina waandaa vijana kuwa wawajibikaji katika familia zao.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *