UBAGUZI KWENYE FAMILIA CHANZO CHA UKIMWI

Katibu wa Baraza la Watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (VVU) NAKOPHA Konga Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza Joseph Kiharata ameitaka jamii kuweka usawa katika familia ili kuwaepusha wanawake na maambukizi ya Virusi vya ukimwi.

Kiharata amesema ubaguzi katika familia hasa wa kiuchumi unaweza kusababisha wanawake kupata maambukizi ya VVU.

”Moja ya sababu ambayo inaweza ikampelekea mdada au mama kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi uchumi pia ni sehemu moja wapo”.

”Binti kama atakosa kipato kuna wakatimwingine anamahitaji yake ya muhimi ambayo kimsingi na yeye anataka ayafanye kwahiyo kama hana kipato tafsiri yake atakwenda kumvamia mbaba asiye jua haliyake ya maambukizi…lakini chanzo tumeona kwamba kipato kwenye familia kilikuwa kidogo aidha familia ilimtenga kwasababu yeye ni mtoto wa kike”amesema Kiharata.

1 thought on “UBAGUZI KWENYE FAMILIA CHANZO CHA UKIMWI”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *