WANASIASA WATAKIWA KUTUMIA LUGHA ZA STAHA

Ikiwa mtu yoyote atatumia lugha isiyo Rafiki kwenye uchaguzi ataadhibiwa kwa mujibu ya sheria.

Hayo yamebainishwa na wakili wa kujitegemea, Kanani Chombani akizungumza na afya redio akiwataka wanasiasa kutumia kanuni za maadili kwa kufuata sheria za uchaguzi na sheria za nchi.

Amesema ikiwa mgombea atanyanyaswa kijinsia, anatakiwa kufuata utaratibu ili muhusika achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria inavyotaka.

Bw. Chombani ameitaka jamii kujiepusha na ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake wakati huu tunapoelekea kwenye chaguzi mbalimbali hapa nchini

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *