Madereva 16 wafungiwa leseni

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafugwa akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari Jijini Mwanza 30.12.2024.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafugwa amesema Madereva 16 wamefungiwa leseni kwa kipindi cha miezi Sita kwa Mwaka 2024.

Akitoa Taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda Mutafungwa amesema Makosa 15,307 ya Barabarani yamekamatwa kwa kipindi cha tarehe 1, hadi tarehe 30,12,2024 ikilinganishwa na Makosa 13921 yaliyokamatwa kipindi cha tarehe 1,hadi 31.12.2023 ambao madereva 6 walifungiwa leseni

Pia Amesema Magari 17 ya kubeba abiria yamezuiliwa kuendelea na safari katika kipindi cha mwezi mmoja baada ya kukaguliwa na kugundulika kuwa na Ubovu.

Aidha amesema jeshi la polisi linaendelea kuimarisha Ulinzi Maeneo yote Mkoani Humo.

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza pia Limemkamata Mwalimu wa kujitolea Shule ya Msingi Nyanghomango Mkazi wa Mkolani kwa kumbaka Mwanafunzi wa darasa la sita.

Katika hatua nyingine Charles Kasela Makula (62) Mkulima Mkazi wa Mwasegela Mkoani Mwanza ameuawa kwa kupigwa na kitu butu sehemu mbalimbali za mwili.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *