Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amewataka Vijana kutoka Vyuo Vikuu na vya Kati Mkoani humo kuacha tamaa ya mali ambzo hawana uwezo nayo kwani inachochea ukatili wa kijinsia.
Mtanda ametoa rai hiyo mapema leo wakati akizindua Kampeni ya Kampasi Salama inayotekekezwa na Serikali kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Halikadhalika, ametumia jukwaa hilo kuwasihi vijana kujiepusha na makundi hatarishi yanayoweza kuwapeleka kwenye hatari ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia na amewataka kutumia wakati vema kwa ajili ya kuwa salama na kujibidiisha katika masomo.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa UNESCO Nchini Tanzania, Bw. Michael Toto amesema wamedhamiria kutokomeza kabisa ukatili kwa wanafunzi wawapo kwenye kampasi zao na ndio maana wameamua kutoa elimu ya umuhimu wa usalama wa watoto wawapo chuoni kwa ufanisi katika masomo.