Matumizi ya dawa kiholela ni sababu ya usugu wa vimelea vya magonjwa na kupelekea vifo na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
Akizungumza na Afya Radio Mkaguzi wa dawa na vifaa tiba kutoka Mamlaka ya dawa na Vifaa tiba TMD kanda ya ziwa Mashariki Hawa Sabura amesema wapo watu ambao wamekuwa wakitumia dawa bila kufuata utaratibu kutoka kwa wataalamu wa afya.
Amesema wapo watu ambao wananunua dawa bila utaratibu na Kutomaliza, kuzidisha au kupunguza dozi hivyo kupelekea usugu wa vimelea.
Amewasisitiza wataalamu katika maduka ya dawa kufuata maadili na weledi katika kutoa huduma ili Kulinda afya ya jamii.
Pia Wafugaji wanaotumia dawa za binadamu kutibu mifugo wametakiwa kuacha kwani zipo mifugo.