Binadamu mara zote anazo hatua anazopitia katika makuzi yake. Hii ni pamoja na ile ya kuanzia pale anapozaliwa akiwa na umri wa siku sifuri na kuendelea.
Hatua hizo za malezi ni kama mfano wa mkulima apandaye mbegu ardhini akitarajia siku moja atavuna mazao bora.
Kwa wazazi wengi wa siku hizi, ni wazi mtoto anayefaulu darasani, asiyemsumbua mzazi, ndiye anayegeuka kuwa kipenzi cha wazazi.
Feliciana Manyanda ameandaa taarifa ifuatayo kutoa picha kwamba Nini kinatokea mzazi/mlezi anapendelea mtoto mmoja kati ya wengi alionao.