N.C.U yakabidhiwa akaunti yenye zaidi ya sh. bil 1

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda leo amewakabidhi rasmi uongozi wa chama cha Ushirika Nyanza (Nyanza Cooperative Union Limited) N.C.U akaunti Maalum maarufu kama ESCROW iliyo na zaidi ya shs bilioni 1 na kuwataka kufanya matumizi sahihi na yenye tija ya kuendeleza chama hicho.

Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa, ya kukabidhi akaunti hiyo Mtanda amesema Serikali imekuwa na nia njema tangu ilipozuia matumizi ya fedha hizo mwaka 2018 na sasa baada ya kukamilika kwa mifumo ya usimamizi imezirejesha.

Amesema hatosita kuchukua hatua endapo atabaini ubabaishaji wa matumizi ya fedha hizo na kuwataka kuandaa mpango kazi  wa matumizi yanayo kwa lengo la kukiinua chama hicho.

Amesema Serikali ina maono juu ya N.C.U na kwamba inazidi kuwa chombo madhubuti cha kiuchumi hasa kutokana na wingi wa mali zake vikiwemo viwanda.

Naibu Mrajisi wa vyama vya Ushirika nchini Bw. Collins Nyakunga ameishukuru Serikali kwa kuitikia ombi la kurejeshewa akaunti hiyo na kuonesha imani kwa uongozi wa Nyanza kuja na mikakati madhubuti yenye kuleta mageuzi ya kiuchumi.

Amesema Ofisi ya Mrajisi wa vyama vya Ushirika itaendelea kuwa karibu na N.C.U kuhakikisha kunakuwa na usahihi wa matumizi ya fedha hizo.

Nae Mwenyekiti wa bodi ya chama cha Ushirika Nyanza,Benjamini Mikomangwa amesema ni wajibu wao kuweka mipango yenye tija kwa chama hicho baada ya mali zote zilizouzwa kinyume na utaratibu kurejeshewa,

Aidha, Tangu Serikali kuzuia matumizi ya akaunti ya chama hicho mwaka 2018 kwa muda wote huo ilikuwa chini ya usimamizi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *