Sonko Waziri mkuu Senegal

Rais mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye amemteua kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo, Osmane Sonko kuwa waziri mkuu ikiwa ni uteuzi wake wa kwanza kama rais.

Akizungumza mara tu baada ya uteuzi wake, Sonko amesema atawasilisha orodha ya mawaziri anaowapendekeza kwa Rais Faye kwa ajili ya idhini yake.

Waziri Mkuu huyo mpya, amewahi kuwa mshauri wa kisiasa wa Rais Faye na hivi karibuni waliachiwa wote kutoka gerezani muda mfupi kabla ya kufanyika uchaguzi mwezi uliopita.

Wanasiasa hao walipata msamaha, pamoja na wafungwa wengine wengi wa kisiasa kutoka kwa Rais aliyemaliza muda wake Macky Sall.

Awali, Sonko alikuwa anatajwa kuwa mgombea mwenye ushawishi hatua iliyosababisha kutangazwa kuwa hana sifa ya kugombea nafasi ya urais na kusababisha maandamano nchini humo.

Sonko na Faye walifanya kampeni kwa pamoja chini ya kauli mbiu “Diomaye ni Sonko” na Sonko akawataka wafuasi wake wampigie kura Faye ambaye hatimaye alishinda kwa asilimia 54 katika raundi ya kwanza.

Sonko alikuwa mpinzani mkubwa wa rais wa zamani Macky Sall na ana umaarufu mkubwa miongoni mwa vijana wa nchi hiyo ila alikuwa na marufuku ya kushiriki uchaguzi huo kutokana na kesi inayomkabili mahakamani.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *