Mawaziri watakiwa kujibu hoja ripoti ya CAG

Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka mawaziri kujibu hoja zilizoibuliwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akizungumza leo leo katika hafla ya uapisho ya viongozi mbalimbali wateule, wakiwamo wakuu wa mikoa na manaibu Waziri Ikulu jijini Dar es Salaam Rais Daktari Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wateule kuwa nguzo kubwa katika kutatua migogoro iliyopo kwenye jamii.


kwenye uapisho huo wa viongozi wateule, Pia Rais samia amesema mabadiliko ya kiuongozi ni mambo ya kawaida, ili kuimarisha ufanisi katika utendaji kazi kwa jamii.

Vilevile ametaja sababu za uteuzi wa Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha huku akieleza anachokitegemea katika utendaji wake mkoani humo na kwamba Makonda amefanikiwa katika kukichangamsha Chama cha mapinduzi CCM

Aidha katika uapisho huo Rais Samia Suluhu Hassan amemuapisha aliyekuwa Naibu Waziri wa Tamisemi, Deogratusi Ndejembi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu  na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *